• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

DC awataka watendaji kukamilisha miradi ya elimu

Posted on: December 24th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hashim Mgandilwa amewataka watumishi sekta ya elimu hasa wanaosimamia miradi ya elimu katika kata na vijiji waliokwenda likizo, likizo zao zisitishwe na warudi Kwa ajili ya kusimamia vyumba vya madarasa, madawati, viti na meza katika shule zilizopo katika kata na vijiji vyao.

Amesema hayo wakati wa kikao na watendaji wa kata, vijiji na waratibu elimu kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kilichofanyika tarehe 24/12/2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya 


“Hamkupaswa kwenda likizo kabisa kwani agizo la Waziri Mkuu lipo wazi na kwa kwenda likizo ina maana ya kukaidi maagizo na maelekezo ya viongozi wakuu wa serikali” amesema Mgandilwa.

Pia alisema ni wajibu wa kila Mtendaji wa vijiji kuitisha vikao vya ndani na mikutano mikuu ya hadhara Kwa kushirikiana na wenyeviti wa serikali za vijiji ili kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi kutimiza wajibu wao katika kufanya shughuli za maendeleo kwenye  maeneo yao.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndg. Frank Fabian Chonya amewataka watendaji hao kuacha kuishi kwa mazoea na kufuata maagizo yanayotolewa na viongozi wakuu.

“Acheni kuwajibika kwa mazoea siwezi kuwa naagiza alafu nyie hamtekelezi maagizo yangu, tuache hizi tabia tuwajibike tutekeleze maagizo ya viongozi” amesema Chonya

Mkurugenzi aliwataka waratibu elimu kata kusimamia miradi ya elimu katika maeneo yao na  na kuwataka kuibua miradi na ile ambayo haijaisha taarifa zake zipelekwe kwake  kwa maandishi. Alisisitiza kukamilishwa Kwa miradi yote bila kujali ilianza lini.

Naye Mwanasheria wa Halmashauri Albert Mwombeki amewataka watumishi ambao wana kusanya fedha za serikali kwa kutumia mashine za kielektroniki kukusanyia mapato na kuacha kujikopesha fedha za serikali kwani ni kosa kubwa ambalo halivumiliki. Aliendelea kusema akigundulika mkusanya mapato ametumia fedha alizokusanya atambue kuwa  mkono wa serikali utamkuta popote alipo. Aliwaasa watendaji hao kuwasilisha fedha benki kila wanapokusanya na si kukaa nazo au kujikopesha.


MWISHO

Matangazo

  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA KWA SHULE ZOTE ZA WILAYA YA RUANGWA 2021 December 17, 2020
  • TANGAZO LA KUUZA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA May 25, 2018
  • Tangazo la ujenzi wa hospitali ya Wilaya wodi ya wazazi January 21, 2019
  • matokeo ya kidato cha nne 2018 January 24, 2019
  • Ona zote

Habari mpya

  • DC awataka watendaji kukamilisha miradi ya elimu

    December 24, 2020
  • Wafugaji acheni ubabe- Mhe Ndaki

    December 22, 2020
  • RC aagiza kumalizwa kwa mgogoro wa aridhi Mbute na Nangurugai

    December 17, 2020
  • DC Afanya ukaguzi wa vyumba vya madarasa mapya

    December 16, 2020
  • Ona zote

Video

RAIS MAGUFULI AZINDUA UJENZI WA FLY OVER UBUNGO
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa