Utaratibu wa ujazaji wa Fomu za Bima ya Afya (NHIF).
Idadi ya watu wanaotakiwa kujazwa kwenye fomu ya bima ya afya ni 16 kwa mtiririko ufuatao;
ØMchangiaji mwenyewe na mwenza wake(mke au mme)
ØFaili ya watoto wasiozidi 4 chini ya miaka 18,au wazazi/wakwe katika idadi hiyo ya watu wane(40 maana unaweza ukawajaza watoto wawili(2) na wazazi (2).
1. VIAMBATANISHO
vMchangiaji:
1.Hati ya kupokelea mshahara(salary slip) yenye makato ya bima ya afya.
2.Picha zenye ukubwa wa pasipoti(passport size) moja ya hivi karibuni.
vMwenza(Mke au mme)
1.Nakala ya cheti cha ndoa (copy)
2.Picha zenye ukubwa wa pasipoti(passport size) moja ya hivi karibuni.
vWatoto:
1.Nakala ya Vyeti vya kuzaliwa(copy).
2. Picha zenye ukubwa wa pasipoti(passport size) moja ya hivi karibuni.
vWazazi:
1.Cheti cha kuzaliwa cha mchangiaji (mtumishi).
2 Picha zenye ukubwa wa pasipoti(passport size) moja ya hivi karibuni
vWakwe:
•Kuongeza mtegemezi:
Viambatanisho ni vilevile saraly slip,picha pasporti size na nakala ya cheti cha kuzaliwa.
Utalipia benki Tzsh 20,000/=kwa kila kadi iliyopotea kwa akaunti namba 61010016954 yenye jina Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Baada ya hapo utamwona Mratibu ukiwa na loss Report ya polisi,pay slip ya benki uliyolipia na picha passport size ili ujaze fomu nyingine uweze kupata kadi nyingine.
üKwa wastaafu:
Viambatanisho
1.Nakala ya kibali cha kustaafu
2.Unarudisha kodi ulizopewa pamoja na wategemezi wako.
3.Picha yako passport size pamoja na ya mwenza wako ya hivi karibuni ili uandaliwe kadi nyingine.
4.Kama kuna kadi zimepotea kati ya kadi sita(6) ulizopewa,utaripoti kwa mratibu wa Bima ya Afya au Afisa Utumishi ili uandikiwe barua ya kwenda nayo polisi.
DR JOSHUA KILEO 0786511418/ 0714599144
MRATIBU WA BIMA YA AFYA(W) RUANGWA
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa