Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hashim Mgandilwa ameagiza vijiji vilivyopo Wilaya ya Ruangwa kutunga sheria ndogo na kuzitumia kwa kufuata taratibu.
Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na wanakijiji wa kata ya matambalale alipofanya ziara yake ya kikazi Leo 09/10/2018 katika vijiji vinne ambavyo ni Nandandala, Namkatila, Matambalale kusini, Matambalale kasikazini na
Ameagiza hivyo kutokana na kero iliyotajwa na wananchi wa Wilaya hiyo ya kuvamiwa kwa wafugaji na kufanyiwa uharibifu wa mazao katika mashamba yao.
Mkuu wa Wilaya amesema kila mtanzania anahaki ya kuishi katika eneo lolote lilipo ndani ya Tanzania Ila anapaswa kufuata sheria na taratibu za eneo husika.
"Mimi simkatazi mtu kuhamia ndani ya Wilaya ya Ruangwa ila unaehamia anapaswa kufuata sheria za eneo husika usitake kuhamia eneo la watu alafu ukajidai wewe mjuaji na kudharau serikali ya kijiji" amesema Mgandilwa
Aidha mheshimiwa amesema hatomvumilia mfugaji anaepeleka mifugo yake katika mashamba ya watu na akalisha mifugo hiyo nikipata kesi kama hiyo nitakushughulikia.
"Nakuanzia kusimamia hilo kila mfugaji akaripoti katika serikali ya kijiji atoe taarifa zake zote zitakazoitajika na ikitokea kijiji kimejaa ukiambiwa hautopokelewa uondoke Mara moja mkatafute eneo jingine na huo ndiyo uwe utaratibu wa kila mgeni anaehamia.
"Serikali ya kijiji ni lazima iwe na sheria ndogo itakayowaongoza kufanya maamuzi na kufuata taratibu za kisheria mkiwa na sheria ndogo hakuna mtu atakae wasumbua mkitaka kumchukulia hatua kwani mtakuwa mnasimamia sheria" amesema Mgandilwa
Naye mfugaji Shoo Bahaini alikiri kuwepo na uharibifu na mazao ya wakulima yanasababishwa na kitendo cha mfugaji kulisha ng'ombe zake katika mashamba ya watu yenye mazao.
Pia Shoo alisema si kila mfugaji ni mkorofi ni watu wachache wanaowaharibia jina hivyo aliwaomba wakulima kuangalia chapa ya ng'ombe atakayomkuta anakula mazao yake alafu akashitaki sehemu husika.
Amesema mfugaji shoo sisi tunaipenda Ruangwa na tunania ya kuishi kwa amani Ruangwa tuko tayari kushirikiana na wakulima wanaoharibiwa mazao yao na wafugaji ambao si waaminifu tunataka kuwe na amani kati ya mfugaji na mkulima.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa